Nimechoka na mambo ya uwajibikaji. Nilitaka kuandika chochote kuhusu muziki. Lakini jana nilisoma Ndesanjo Macha na changomoto yake kuhusu ukombozi wa Afrika. Bonyeza hapa. Mambo mengi ya kufikiria.
Leo nimebahatika kusoma mahojiano ya Femi Kuti kwa LA Weekly. Bonyeza hapa ukitaka kusoma maneno yake (kwa njia ya Ethan Zuckerman).
Ukiwepo Los Angeles Ijumaa ijayo, usikose kuhudhuria shoo yake. Nilihudhuria mara moja Ulaya nikacheza mpaka basi…..
July 25, 2007 at 8:31 pm
Femi weka pembeni. Mdogo wake anayeitwa Seun utadhani Fela Kuti karudi duniani. Nasikia ndugu hawa wawili haziivi…sina uthibitisho. Ni zile redio za mtaani. Nasikia kila mmoja anataka kusema kuwa ndio mrithi hasa wa baba yao kimuziki. Lakini Seun kamchukua Fela kabisa: uvaaji akiwa jukwaani, midundo ya muziki wake, uimbaji, uchezaji, umachachari, n.k.
July 25, 2007 at 9:21 pm
Kweli, nilicheza mpaka basi siku ile. Lakini pia nilisikitika kidogo. Femi amefuata hatua za baba, lakini amebana mtindo wake. Yaani, amechukua zile ‘highlights’ za mtindo wa baba. Lakini muziki wa baba siyo wa kucheza-cheza tu. Alizoea kutumia muda mrefu kwenye saxophone au kinanda – tungetafakari pamoja naye.
Soma maneno ya femi mwenyewe kwa http://www.npr.org/templates/story/story.php?storyId=11835088
“I wanted to do something very compact so that it wouldn’t bore the new listener,” Femi says. “Because imagine somebody who is not an Afro-beat lover. You have to catch their attention immediately. My father’s songs were more for fanatics and for people who heard him over the years and heard his transformation, and those people are ready to listen to forty-five minutes or even an hour. But somebody who is going to listen to Afro-beat for the first time, what’s going to catch his attention? Why would he want to go through an hour of listening to numbers, because he’s already used to R&B, he’s used to be-bop, he’s used to hip hop, he’s used to rock, he’s not going to want to sit down anywhere for one hour listening to one track.”
July 26, 2007 at 5:15 pm
Tatizo ni kwamba, tumjuaye Fela , ni lazima tutataka kuwafananisha watoto wake na yeye.Ila nilicheki video clips fulani za Seun akipiga nyimbo za baba yake, kama kipofu unaweza kufikiri ni Fela karudi.
July 26, 2007 at 5:41 pm
Asante Katibu. Tatizo langu ni kwamba, siku ile kwenye shoo, nilisikitika zaidi kwa jinsi Femi alivyofanana na baba yake. Mimi nampenda sana marehemu baba yangu, lakini sioni faida ya kufuata nyayo zake kamili. Nilipomaliza masomo yangu, alisema “basi, kazi yangu imekwisha. Sasa ni kazi yako ya kuendesha maisha yako”. Yaani, alinipa uhuru ya kufanya maamuzi yangu kama mtu mzima.
Ningefurahi zaidi Seun na Fela waendeleze kazi ya marehemu baba yao mbele zaidi kuliko kupiga copy tu.