Je, umeshasoma ripoti ya Mwakyembe? Si unajua jinsi viongozi walivyokula? Dakika arobaini zilizopita, wabunge walikubali uteuzi wa Mizengo Pinda, Mbunge wa Mpanda Mashariki, kama Waziri Mkuu. Walimsifia. Walimpa moyo. Aliwashukuruu. Sitta alifunga kikao kwa mtindo wake. Lakini kumbe, alipewa karatasi kutoka kwa mmoja wao. Mbunge huyo alikuwa na swali….. “je, sherehe ya kumpongeza Waziri Mkuu itafanyika lini?”
Kashfa ya siku hizi ilielekea kuvunja siasa yetu. Mbunge huyo anafikiria nini? Chakula tu!
February 16, 2008 at 8:50 pm
watanzania wengi sasa tumefumbuka macho kwani muda muafaka umefika kwa wananchi kujua haki zao za msingi. Hatuna budi kuungana na kuwa kitu kimoja. Kwa sasa mafisadi hawana chao.