Basi, nimeanza sasa. Sijui kama blogu hii itaendelea kwa kiingereza au kiswahili, lakini lazima nianze sasa.

Nianze kwa vyombo vya habari, hasa udaku. Kusoma udaku ni moja ya “guilty pleasures” zangu. Na wewe, je? Zinachekesha, zinashtua na maajabu yao. Siku za kwenda mbele, nadhani utasoma tafsiri mbalimbali za stori zao. Lakini tusizikubali kabisa. Pamoja na kuchekesha, zinachafua watu mbalimbali na uongo wao.

Jana nilisoma hii kwa African Entrepreneur. Amesimulia hadithi yake ya kuchafuliwa na udaku kwao. Kwanza, walianza na stori fupi kufahamisha wasomaji kuwa wangetangaza ‘ukweli’ kuhusu mama huyo wiki iliyofuata. Nia yao, walitaka asome hii habari, awatafute kwa ajili ya ‘maelewano’, yaani, awalipe wasitangaze. Hakulipa walitangaza uongo, basi.

Nilikumbushwa na harakati za Miss Tanzania na staa fulani ya Bongo Flava (miezi mitatu iliyopita?). Gazeti moja walitangaza kuwa walikuwa na picha zake, hawakutaka kuzitangaza wazi kwa sababu ya uchafu wao. Baada ya wiki moja, picha zilitangazwa.

Je, walikuwa wanatangaza kwamba “picha zipo, njoo Miss Tz, tuzumgumze. Maelewano yapo”?

Kwa upande mwingine, inajulikana kuwa hapa Tanzania, ukitaka kutangaza shirika, filamu au CD yako (hata mradi yako yakupunguza umaskini), malipo yanasaidia sana. Basi, ndivyo ilivyo, na siyo Tanzania tu.

Kwa udaku, tabia hiyo haishangazi. Lakini kwa upande wa ‘quality press’ – kwa mfano, Majira, Guardian, Citizen, Mwananchi, n.k. – je, mambo yapo tofauti sana kuliko udaku?

Mara nyingi, kazi ya Kulikoni na This Day ni kuchunguza mambo ya Manji. Rushwa ni kwa mtu mmoja tu hapa Tanzania? Mwananchi ina taarifa nyingi kuhusu uchaguzi wa CCM, lakini bila majina kamili. Inasaidia nani? Alasiri, je? Wengi tumesoma taarifa zao chini ya jina la ‘Mwandishi Wetu’. Soma hii hapa. Je, ni tangazo maalum ya Ikulu au Mtaa wa Lumumba, au uandishi wa habari ya kawaida? Na tabia ya udaku, imefika kwa chombo cha habari cha dola.

Kwa hiyo, msomaji mpendwa, tuendelee na kujifurahisha na magazeti zetu. Lakini tusome kwa makini.

Wakati ya kuandika hii, nilisoma Global Voices na taarifa iliyoandikwa na J Nambiza Tungaraza. Namshukuru.

Advertisements