Juu nimeandika ‘Gini’, siyo ‘Jini’. Suala la leo ni mambo ya uchumi, siyo uchawi. Lakini wengi wanasema kuwa uchumi ni aina moja ya uchawi… Basi, tuendelee.

Gini Coefficient ni jinsi moja ya kupima utofauti wa mapato ya watu. Kama Gini co-efficient ni 1, kuna utofauti sana kati ya walala hoi na matajiri. Kama ni 0, mapato ni sawasawa kabisa. Gini co-efficient ya Tanzania, imeongezeka kutoka 0.34 mwaka 1991 mpaka 0.35 mwaka 2001. Inaonyesha kuwa utofauti wa mapato haujabadilika sana, lakini uliongezeka taratibu.

Nadhani kuwa tangu 2001 gini co-efficient imeongezeka tena. Mambo yanabadilika sana siku hizi, hasa mijini. Magari aina ya shangingi, majumba ya dhahabu, BANG! Magazine….. Bila shaka utofauti wa mapato utaongezeka wakati soko huru linakua. Wasomaji wa taarifa mbalimbali kutoka katika mkutano wa TED pale Arusha hivi karibuni, watajua kuwa wengi wanadhani kuwa siri ya maendeleo yetu ni ujasiriamali. Hata mimi nakubali… nadhani.

Swali langu ni hili: je, utofauti wa mapato ni kitu kizuri au kibaya? Mimi sijui jibu. Ukisoma EastSouthWestNorth, utapata maoni mawili tofauti kuhusu suala hili pale Hong Kong, ambapo Gini co-efficient imeongezeka hivi karibuni. Asante kwa EastSouthWestNorth kwa kutafsiri kutoka kichina kwenda kiingereza taarifa hizi za magazeti ya Hong Kong.

Advertisements