Sikutaka kuandika chochote kuhusu skendo ya Benki Kuu ya Tanzania inayohusu “external arrears payments”. Mambo mengi yameshaandikwa.

Juzi nilitembelea tovuti ya IMF kwa ajili ya kujua maoni yao kuhusu Benki Kuu na skendo hiyo. Ukibonyeza hapa, utapata nakala yako ya IMF Country Report No. 07/138: karatasi tisini na saba. Hii ni ripoti ya mwisho ya Poverty Reduction Growth Facility na Policy Support Instrument ya miaka mitatu ijayo. Napendekeza usome. Kuna mambo mengi ndani.

Kusema ukweli, nilishtushwa na ripoti hiyo. Bila shaka wananchi wa Tanzania wamesikitika sana na allegations kuhusu Benki Kuu. Wanaomba uwajibikaji. Je, vyombo vya fedha vya kimataifa vinasemaje? Kwanza, inaonekana kuwa wanaona mambo haya kuwa muhimu, lakini kiasi tu, siyo sana.

Nilishangaa zaidi mahusiano kati ya maafisa ya IMF na wenzao kwa Benki Kuu ya Tanzania. Ripoti hiyo ya IMF, inatueleza nini? Yaani, nani husimamia wasimamizi?

Kwa kweli, akina-IMF hawana mengi ya kusema. Hamna cha kusema mpaka kufikia ukarasa 81 ya 97. Wafanyakazi wa IMF, wanatuambia kuwa walipata taarifa ya “an alleged impropriety” baada ya kumaliza ripoti yao ya mwisho kuhusu PRGF.

Following issuance of the staff report for Tanzania’s sixth and final PRGF review, and request for a three year PSI, the staff learned of an alleged impropriety involving payments to a third party by the BoT. The allegation raised questions regarding program implementation, capacity to repay the Fund, and the consistency of the BoT’s practices with the Fund’s safeguard’s policy, including the BoT’s own commitments following the December 2003 Safeguards Assessment. The alleged impropriety has also given rise to reputational risks for both the fund and the BoT. As a result, Board consideration of the report, scheduled for December 6, was postponed and the PRGF was extended to mid-August 2007 to all the staff additional time to seek from the authorities (i)clarification of the nature of the alleged impropriety; and (ii) reasonable assurances that no systemic problem exists that give rise to safeguards concerns. The staff has also reached understanding on the adoption of remedial actions.

Mambo haya ya malipo yasiyo sahihi, yalichunguzwa na audit firm moja, ambayo, ilifukuzwa na serikali baada ya kueleza mambo haya kwa IMF. Baada ya hapo, tunaambiwa kuwa IMF iliwasiliana na serikali ya Tanzania, mpaka Ikulu. Inaonekana kuwa IMF walikubali maelezo yote ya serikali.

“Remedial actions” hizo, zinaelezwa zaidi ndani ya barua kutoka Mh Zakia Hamdani Meghji, Waziri wa Fedha kwa Mkurugenzi wa IMF, Rodrigo de Rato ya tarehe 8 Februari 2007. Kwa ufupi, serikali inaamini kuwa skendo ni “an isolated occurence”, wameanza uchunguzi wao, na pia, watapata audit firm kutoka nje kuchunguza zaidi.

Mambo haya tunayafahamu, lakini, nilishtushwa zaidi kusoma Statement by Peter Gakunu, Executive Director for United Republic of Tanzania and Joseph L. Masawe, Senior Advisor to the Executive Director”, ambayo ni appendix kwenye ripoti hiyo ya IMF.

Gakunu na Masawe wanatuambia kuwa

Without prejudging the outcome of the audit, my authorities believe that this is an isolated incident and do [sic] not pose reputational or safeguard risks at the BOT. The BOT has been the first institution in Tanzania to become IFRS compliant and remains so.

Yaani, bila kusibiri matokeo ya uchunguzi, wanataka kutoa maoni yao kuwa mambo yanaendelea vizuri.

Mwishoni, Gakunu na Masawe ni akinanani? Gakunu yupo IMF, baada ya kuwa afisa wa ngazi ya juu katika Wizara wa Fedha ya Kenya. Na Masawe? Yupo IMF pia. Kabla ya kuanza kwa IMF, alikuwa Deputy Director wa Bank of Tanzania – akiwajibika kwa na Daudi Balali, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

 

Advertisements