Pew Global Attitudes Project ni mradi ambao unajitahidi kupima mitazamo ya watu duniani kuhusu mambo mbalimbali. Ukitembelea tovuti yao, inaonekana kuwa lengo lake ni kufahamisha viongozi wa siasa wa Amerika mitazamo ya nchi mbalimbali duniani.

Mwezi huu, walitoa matokeo ya utafiti wao wa mwaka huu wa nchi 47, Tanzania ni mojawapo. Ukitaka kuelewa zaidi mradi huu, bonyeza hapa (pia utapata nafasi ya kupata nakala yako kwa download). Kuna mambo mengi ya kutafakari humu ndani. Nachukua fursa hii kuwaonyesha wasomaji wapendwa matokeo machache kuhusu mitazamo ya wananchi wa Tanzania. Matokeo mengi zaidi yanapatikana kwenye ripoti.

Asilimia ya wananchi ambao wamefurahia …

Maisha yao: 10%    Hali ya taifa: 46%    Serikali kuu: 86%

Asilimia ya wananchi ambao wanadhani kuwa maisha ya watoto wao yatakuwa…..

Mabaya zaidi: 47%    Bora zaidi: 36%   Sawa sawa: 9%  

Asilimia ya wananchi ambao wanaona kuwa taasisi yafuatayo yanaleta ushawishi mzuri kwa maendeleo ya taifa….

Viongozi: 95%    Jeshi: 85%    Vyombo vya habari: 86%

Asilimia ya wananchi ambao wanasema kuwa inahitajika watoe rushwa kupata hudumu za serikali….

Mara kwa mara: 14%    Mara chache: 13%    Kamwe: 70%

Asilimia ya wananchi ambao wanadhani kuwa rushwa kwa viongozi ni tatizo kubwa….

68%

Asilimia ya wananchi ambao wanadhani kuwa nchi tajiri zinataka kusaidia Afrika iendelee…

59%

Advertisements