Mwezi uliopita, nilikosa sherehe ya Poverty Week. Imefanyika Ubungo Plaza, kama uzinduzi wa kampeni dhidi ya ‘trafficking’. Shughuli nyingi zimetokea, uzinduzi wa Views of the People 2007 ni mmojawapo.

Views of the People 2007 ilizinduliwa na Prof. Semboja, mkurugenzi wa Research for Poverty Alleviation (REPOA). REPOA ilifanya utafiti huu mkubwa kwa ajili ya kupata maoni ya wananchi kuhusu utekelezaji wa Mkukuta. Walihoji zaidi ya watu 8,000 katika mikoa kumi ya Tanzania bara. Ripoti ni ndefu. Nitaweka matokeo machache tu hapa.

Asillimia ya watu ambao wamesikia Mkukuta                                                38

Asilimia ya watu ambao wanaamini maofisa wa NGOz                                 12

Asilimia ya watu ambao wanaamini polisi                                                         12

Asilimia ya watu ambao wanaamini wanasiasa                                               14

Asilimia ya watu ambao wanadhani watu kwa ujumla wanaaminika         22

Kwenye ripoti hii kuna mambo mengi ya kutafakari. Lakini nashangaa ripoti hapatikani kwa urahisi. Labda REPOA hawawaamini wananchi…. Haionekani kwenye tovuti yao. Haionekani kwenye tovuti ya kitengo cha kupima umaskini cha Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji (pia, tovuti hiyo inapatikana kwa kiingereza tu). Kwanini, jamani? Wamepima maoni ya wananchi lakini wananchi hawana fursa ya kusikia sauti zao wenyewe. Imeshazinduliwa kwa ‘wadau wa umaskini’ kwa sherehe ya Poverty Week. Maskini wenyewe, je?

Advertisements