January 2008


“Utawala bora unalipa.” Haya ndiyo maneno ya Bw. Bertie Ahern, Waziri Mkuu wa Ireland, kwenye hotuba yake kwa wananchi wa Ireland ambao wanaishi hapa Tanzania. Soma hotuba nzima kwa kubonyeza hapa.

Pia, kwenye hotuba hiyo aliwasimulia wageni kuhusu mkutano wake na Rais Kikwete.

I commended the President for the very strong statements he has made on the need to tackle corruption. He acted decisively, openly and publicly following the recent independent international audit on the Bank of Tanzania.

His message to the people of Tanzania, to fellow African countries and to the wider international community is clear: Corruption has no place in a democratic society.

Lakini Bw. Bertie alisahau kuwaambia kuwa wapinzani pale Ireland wamedai kuwa yeye hastahili kuwa Waziri Mkuu kwa sababu chombo kimoja cha dola kinamchunguza kwa kutolipa kodi ya mapato wakati alipokuwa Waziri wa…………. Fedha.

Chanzo cha uchunguzi huo ni uchunguzi mwingine unaohusu mipango ya ardhi. Uchunguzi, unaojulikana kama Mahon Tribunal, umegundua kuwa Bw. Bertie alipokea malipo ya thamani ya zaidi ya Euro60,000 kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali kati ya mwaka 1993-94. Bertie ameshindwa kueleza kwanini walimpa pesa kiasi hicho wakati alikuwa Waziri wa Fedha.  Sasa mamlaka ya kodi ya Ireland wanamchunguza pia kujua kwanini hakulipa kodi ya mapato kwenye malipo hayo. Maelezo zaidi yanapatikana hapa.

Zaidi ya hapo, Bw. Bertie alifagilia umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari alipozungumza na wahariri wa magazeti mbalimbali ya Tanzania. Lakini nilishangaa Bw. Bertie alikataa kujibu swali lolote kuhusu madai ya wapinzani wake wakati wa ziara yake.

Mbona wafadhili wanatufundisha mambo ya utawala bora wakati wao wenyewe wanachunguzwa?

Advertisements

Yafuatayo ni matokeo kutoka kwenye Centre for Global Development. Utafiti huu, wa Michael Clemens na Gunilla Pettersson, ulihusiana uhamaji wa madaktari na manesi kutoka Afrika. Matokeo ni ya mwaka 2000 kwa sababu utafiti huo ulilinganisha matokeo ya sensa za nchi mbalimbali.

Idadi ya madaktari Tanzania                          1,264

Idadi ya madaktari ambao wapo nje             1,356

Idadi ya manesi Tanzania                             26,023

Idadi ya manesi ambao wapo nje                     953

Je, uhamaji wa madaktari unaathiri huduma za afya hapa Tanzania? Pia, kwanini manesi wamebaki nyumbani?

Matokeo yote yanapatikana hapa. Nimeyapata kwa njia ya Dani Rodrik.

Duh! mambo ya usimamizi hayana mwisho, au siyo?

Tumesikia vigelegele na makofi hivi karibuni. Sio ya harusi ama sherehe ya aina yeyote. Wala. Tumyaesikia wafadhili kuipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka wazi matokeo ya audit External Payments Account nawa wizi wa zaidi ya dollar milioni mia moja kutoka Benki Kuu ya Tanzania . Juzi, Daudi Balali, gavana mwenyewe alifukuzwa.

Mark Green, balozi wa Marekani hapa Tanzania alisema: “We believe that the government’s decision to press forward with an investigation of irregularities at the bank is indicative of President Kikwete’s resolve to combat corruption”. Serikali ya Uingereza pia, waliunga mikono na Bw. Green.

Tunajua kuwa audit ya Ernst and Young sio audit ya kwanza. Lakini uchunguzi huo si uchunguzi wa kwanza bali ni uchunguzi wa pili……. Endelea kusoma.

IMF iko mstara wa mbele wa kero hii ya BoT. Nimeshaandika kuhusu IMF na BOT. Bonyeza hapa ukitaka kujikumbusha. Kwenye nakala ile, niliunganisha na Country Report No. 07/138. Pata nakala yako hapa tena. Ni bure.

Leo mimi nimeisoma tena, kujikumbusha skendo hiyo. Ilivyoandikwa kwenye ripoti ya IMF, mambo yafuatayo yalitokea:

  1. Mwaka 2006, maodita wa Benki Kuu ya Tanzania (Deloitte and Touche, kama sijakosea), waligundua malipo ya thamani ya USD30.7 milioni ambayo siyo sahihi.
  2. Mkataba ya maodita ulivunjwa na serikali
  3. Akina-IMF walipata taarifa kutoka kwa maodita wa Benki Kuu kuhusu malipo hayo.
  4. Akina-IMF waliwasiliana na serikali juu ya kero hiyo kwa ngazi za juu, hadi Rais na Waziri wa Fedha
  5. Serikali ya Tanzania iliwaambia IMF kuwa malipo haya yalitokea External Payments Account
  6. Februari 2007, Waziri wa Fedha aliahidi kuchunguza malipo husika kwa njia ya ‘audit’ mpya.
  7. Zaidi ya ‘audit’, serikali ilianzisha unchunguzi mwingine wa malipo. Huu umeanzishwa kabla ya Februari 2007, kama Waziri wa Fedha alivyoandika kwenye barua yake kwa Rodrigo Rato wa IMF, ambaye ni appendiz kwenye Country Report ya IMF.

Juzi, tulipewa matokeo machache (sio yote) ya audit ya Ernst and Young (au Massawe Ernst and Young? Sina uhakika…..). Tulipewa majina ya makampuni mbalimbali ambayo walipokea mabilioni kutoka kwa External Payments Account ya Benki Kuu. Tumehakikishiwa kuwa serikali itaunda timu ya kuchunguza mambo hayo. Timu, wakiwemo Inspekta Jenerali, na mkurugenzi wa Takukuru, Itaongozwa na mwanasheria mkuu.

Vipi kuhusu uchunguzi wa kwanza, je? Je, walishindwa kupata majina ya kampuni zilizopokea fedha hizo mpaka odit ya hivi karibuni?

Pia, kwanini wafadhili wanaipongeza serikali kwa kuunda uchunguzi sasa? Si wanajua kuwa serikali iliuunda uchunguzi karibu na mwaka moja uliopita?

Gazeti la MwanaHalisi halina tovuti, lakini blogu za Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage zinaonekana hapa na hapa.

Dani Rodrik ni mchumi maarufu duniani. Pia ni mwalimu mwenye vipaji. Kwa bahati nzuri, ni mwanablogu pia. Ukitaka kujua uhusiano kati ya taa za kuongozea magari na utawala bora, napendekeza usome nakala yake moja kwenye blogu yake. Iko hapa. Hutasikitika kwa kusoma na hasa kutazama video viwili vilivyounganishwa kwake.

Hapa Tanzania, tumeachwa kwenye mataa? Ukitazama mfumo wa magari hapa Dar es Salaam, utajifunza nini kuhusu mambo ya utawala bora hapa Tanzania?

Mwezi uliopita, niliungana na nakala moja ya Ndimara Tegambwage kwa gazeti ya Daima. Nimesikitika pia nimekasirika kusoma kuwa jana Tegambage na mhariri wa MwanaHalisi, Saed Kubenea, wamepigwa ndani ya ofisi ya MwanaHalisi. Tegambwage ni mwanablogu pia. Soma ripoti ya This Day kwa kubonyeza hapa.

Mimi siwafahamu Tegambwage na Kubenea. Sijui kama wameandika ukweli au uongo. Tumefikia wapi?

Sasa nakala yangu inaonekana kwenye tovuti ya JBN. Soma hapa. Matangazo mawili yapo, kwa International School Moshi na Kili Treks Safari. Nasubiri kipato changu……..

Next Page »