“Ukimwi Day imeisha – tunasubiri Uhuru Day.” Maneno haya niliambiwa leo, na pia yana maana. Hapa Tanzania tunapewa ujumbe juu ya ujumbe “kila dakika, kila saa, kila saa, kila siku” (asante II Proud). Kama siyo Ukimwi, ni Uhuru. Kama siyo Uhuru, itakuwa mapambano dhidi ya rushwa.

Kila ujumbe umependekezwa na ngazi za juu. Kama siyo serikali, ni wafadhili. Tutasikia lini sauti ambazo zinaleta ujumbe wa ukweli kutoka moyoni? Tutasikia lini sauti ambazo zinatuletea vitu vipya, ambavyo vitatusisimua kwa ukweli na nguvu zao?

Je, tutapata nafasi hiyo?

Advertisements