constitution


Ukipata nafasi, tembelea blogu ya Jumuwata. Wameomba tuchangie mawazo yetu kuhusu katiba mpya ya Jumuwata.

Hapa Tanzania, tumezoea kushirikiana kwa mabaya na mazuri. Lakini Jumuwata ni kitu kipya, ambacho tunajitahidi kushirikiana bila kukutana rasmi.  Sote tumekaribishwa. 

Advertisements

Leo, inasomekana kwenye Daily News kuwa serikali haina uwezo ya kutangaza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi.

We have to make people understand the importance of the constitution before we can think about making it available to everyone for free,” said Dr Nagu in response to Dr Festus Limbu (Magu Urban-CCM), who had earlier suggested that the document be distributed freely to all government institutions and non-governmental organisations (NGOs) all over the country.

Tafakari…..

Baada ya kutafakari kidogo, nilipata Katiba hapa, nilisoma yafuatayo:

8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo –
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao
kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Je, wananchi wafahamishwe umuhimu wa Katiba kabla ya kusoma? Je, wananchi ni msingi wa mamlaka wote bila kusoma Katiba?