Baada ya kununua kiwanja cha mtu, inabidi ubadalishe jina kwenye hati. Hatua ya kwanza ni afisa wa serikali akadirie thamani ya ardhi. Kodi ya mauzo inategemea na thamani hiyo. Bila taarifa ya thamani ya ardhi, haiwezekani kubadalisha majina kwenye hati. Bila kubadalisha majina, haiwezekani kupata kibali cha ujenzi. Bila ujenzi, hamna nyumba. Safari ni ndefu.

Kiasi gani kinahitajika kukadiria ardhi? Maelewano yapo……. tulitoa TZS100,000, risiti iliandikwa kwa TZS2,000.

Hii ni hatua ya kwanza. Mambo yataendelea.

Advertisements