police


Kaka Michu, nisiseme kuwa mimi ni mshabiki wa blogu yako. Lakini ukweli, nimeitembelea mara nyingi. Labda unajua kuwa nimeandika makala kuhusu blogu yako mara moja au mbili. Kama umesahau, bonyeza hapa.

Mimi hutembelea kwako kwa sababu naona unavutia watu wengi sana duniani. Na kweli, nakupongeza kwa kazi yako nzuri ya kuunganisha waswahili duniani. Hamna mwingine ubloguni kwetu kama wewe. Hongera.

Lakini kila mtu ana mapungufu yake. Hata mimi, na wewe pia, anko. Jana, nilisoma makala moja kwako ambayo imenisikitisha sana. Ilihusiana na mwanablogu moja hapa Tanzania anayeitwa Pernille. Wengine wabonyeze hapa wakitaka kuisoma (hata wewe kama umesahau). Kwenye makala hiyo, mtu fulani, kwa jina la ‘Suby’ amelalamika kuhusa makala ya Pernille. Pernille alikuwa akielezea mambo ya foleni za magari hapa Dar es Salaam. Alimtaja trafik wa kike kuwa na “legs like small tree trunks”.

Sawa. Lakini, jana pia, umetangaza makala nyingine. Kama umesahau (najua upo bize sana), bonyeza hapa. Ulitangaza barua au tangazo kutoka kwa mtu asiyejulikana ambaye alitaka kutangaza kundi ya facebook ya kugomea blogu ya Pernille. Kwenye picha iliandikwa “Apologise or Leave!!”. Ametukaribisha sote tuungane naye.

Lakini, Michuzi, hujatuambia kwanini tuungane naye. Hujatuambia kwanini a-“apologise or leave!!”. Wewe umekaa kimya. Hakuna ya kuangalia ila tabasamu lako kwenye picha yako nzuri kwenye tovuti. Kwa ukimya wako, umeunga mkono asili mia kwa mia na muundaji wa kundi. Wewe uliweka bango lao kwenye blogu yako. Wewe umemwambia Pernille “Apologise or Leave!!”

Nadhani wewe uombe msamaha kwa Pernille. Pia napendekeza uondoe makala ya pili, ulivyoondoa makala kuhusu Global Scouting Bureau mwaka uliopita.

Advertisements

Mwezi uliopita, nilikosa sherehe ya Poverty Week. Imefanyika Ubungo Plaza, kama uzinduzi wa kampeni dhidi ya ‘trafficking’. Shughuli nyingi zimetokea, uzinduzi wa Views of the People 2007 ni mmojawapo.

Views of the People 2007 ilizinduliwa na Prof. Semboja, mkurugenzi wa Research for Poverty Alleviation (REPOA). REPOA ilifanya utafiti huu mkubwa kwa ajili ya kupata maoni ya wananchi kuhusu utekelezaji wa Mkukuta. Walihoji zaidi ya watu 8,000 katika mikoa kumi ya Tanzania bara. Ripoti ni ndefu. Nitaweka matokeo machache tu hapa.

Asillimia ya watu ambao wamesikia Mkukuta                                                38

Asilimia ya watu ambao wanaamini maofisa wa NGOz                                 12

Asilimia ya watu ambao wanaamini polisi                                                         12

Asilimia ya watu ambao wanaamini wanasiasa                                               14

Asilimia ya watu ambao wanadhani watu kwa ujumla wanaaminika         22

Kwenye ripoti hii kuna mambo mengi ya kutafakari. Lakini nashangaa ripoti hapatikani kwa urahisi. Labda REPOA hawawaamini wananchi…. Haionekani kwenye tovuti yao. Haionekani kwenye tovuti ya kitengo cha kupima umaskini cha Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji (pia, tovuti hiyo inapatikana kwa kiingereza tu). Kwanini, jamani? Wamepima maoni ya wananchi lakini wananchi hawana fursa ya kusikia sauti zao wenyewe. Imeshazinduliwa kwa ‘wadau wa umaskini’ kwa sherehe ya Poverty Week. Maskini wenyewe, je?

Tatizo la ujambazi bado linaendelea hapa Tanzania. Wiki iliyopita, polisi waliua Wakenya 14 mjini Moshi. Pale Nairobi, watu wanauliza maswali. Wanaomba kuwa mauaji yachunguzwe:

All we ask for is thorough investigation into the grisly killings so that the circumstances under which they happened become clear. It is encouraging that the Kenyan and Tanzanian police are working together on the matter.

They should complete the investigations as quickly as is possible and practicable, compile the report and make it public. And the matter should not stop there. Those who will be found to have acted against the law, used excessive force or executed Kenyans must face the full force of the law.

Nilishangaa zaidi kusoma kwamba wanaharakati kutoka Kenya walikamatwa na Polisi Moshi.  Bado sijasikia chochote kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadhamu hapa Tanzania. Kwanini wamekaa kimya?

Je, ni sahihi watu ambao wametuhumiwa kuwa majambazi wauawe kama wanyama porini?  Waziri wa Usalama na Raia, Bw. Bakari Mwapachu hana wasiwasi:

“Jeshi Polisi mkoani Kilimanjaro linastahili pongezi na siyo lawama, waendelee hivyo hivyo na hakuna msalie mtume katika masuala ya uhalifu na uvunjaji wa amani, tumejipanga vyema kukabiliana na majambazi,” alisema.

Haki za binadhamu, zitekelezwe sawa sawa kwa wote, wabaya na wazuri. Vinginevyo, hazina maana.  Tusipongeze Jeshi la Polisi kama hawana uwezo wa kuchunguza jinai, kukamata wahusika na kupeleka kesi zao mahakamani.