thieves


Duh! mambo ya usimamizi hayana mwisho, au siyo?

Tumesikia vigelegele na makofi hivi karibuni. Sio ya harusi ama sherehe ya aina yeyote. Wala. Tumyaesikia wafadhili kuipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka wazi matokeo ya audit External Payments Account nawa wizi wa zaidi ya dollar milioni mia moja kutoka Benki Kuu ya Tanzania . Juzi, Daudi Balali, gavana mwenyewe alifukuzwa.

Mark Green, balozi wa Marekani hapa Tanzania alisema: “We believe that the government’s decision to press forward with an investigation of irregularities at the bank is indicative of President Kikwete’s resolve to combat corruption”. Serikali ya Uingereza pia, waliunga mikono na Bw. Green.

Tunajua kuwa audit ya Ernst and Young sio audit ya kwanza. Lakini uchunguzi huo si uchunguzi wa kwanza bali ni uchunguzi wa pili……. Endelea kusoma.

IMF iko mstara wa mbele wa kero hii ya BoT. Nimeshaandika kuhusu IMF na BOT. Bonyeza hapa ukitaka kujikumbusha. Kwenye nakala ile, niliunganisha na Country Report No. 07/138. Pata nakala yako hapa tena. Ni bure.

Leo mimi nimeisoma tena, kujikumbusha skendo hiyo. Ilivyoandikwa kwenye ripoti ya IMF, mambo yafuatayo yalitokea:

  1. Mwaka 2006, maodita wa Benki Kuu ya Tanzania (Deloitte and Touche, kama sijakosea), waligundua malipo ya thamani ya USD30.7 milioni ambayo siyo sahihi.
  2. Mkataba ya maodita ulivunjwa na serikali
  3. Akina-IMF walipata taarifa kutoka kwa maodita wa Benki Kuu kuhusu malipo hayo.
  4. Akina-IMF waliwasiliana na serikali juu ya kero hiyo kwa ngazi za juu, hadi Rais na Waziri wa Fedha
  5. Serikali ya Tanzania iliwaambia IMF kuwa malipo haya yalitokea External Payments Account
  6. Februari 2007, Waziri wa Fedha aliahidi kuchunguza malipo husika kwa njia ya ‘audit’ mpya.
  7. Zaidi ya ‘audit’, serikali ilianzisha unchunguzi mwingine wa malipo. Huu umeanzishwa kabla ya Februari 2007, kama Waziri wa Fedha alivyoandika kwenye barua yake kwa Rodrigo Rato wa IMF, ambaye ni appendiz kwenye Country Report ya IMF.

Juzi, tulipewa matokeo machache (sio yote) ya audit ya Ernst and Young (au Massawe Ernst and Young? Sina uhakika…..). Tulipewa majina ya makampuni mbalimbali ambayo walipokea mabilioni kutoka kwa External Payments Account ya Benki Kuu. Tumehakikishiwa kuwa serikali itaunda timu ya kuchunguza mambo hayo. Timu, wakiwemo Inspekta Jenerali, na mkurugenzi wa Takukuru, Itaongozwa na mwanasheria mkuu.

Vipi kuhusu uchunguzi wa kwanza, je? Je, walishindwa kupata majina ya kampuni zilizopokea fedha hizo mpaka odit ya hivi karibuni?

Pia, kwanini wafadhili wanaipongeza serikali kwa kuunda uchunguzi sasa? Si wanajua kuwa serikali iliuunda uchunguzi karibu na mwaka moja uliopita?

Advertisements

Tatizo la ujambazi bado linaendelea hapa Tanzania. Wiki iliyopita, polisi waliua Wakenya 14 mjini Moshi. Pale Nairobi, watu wanauliza maswali. Wanaomba kuwa mauaji yachunguzwe:

All we ask for is thorough investigation into the grisly killings so that the circumstances under which they happened become clear. It is encouraging that the Kenyan and Tanzanian police are working together on the matter.

They should complete the investigations as quickly as is possible and practicable, compile the report and make it public. And the matter should not stop there. Those who will be found to have acted against the law, used excessive force or executed Kenyans must face the full force of the law.

Nilishangaa zaidi kusoma kwamba wanaharakati kutoka Kenya walikamatwa na Polisi Moshi.  Bado sijasikia chochote kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadhamu hapa Tanzania. Kwanini wamekaa kimya?

Je, ni sahihi watu ambao wametuhumiwa kuwa majambazi wauawe kama wanyama porini?  Waziri wa Usalama na Raia, Bw. Bakari Mwapachu hana wasiwasi:

“Jeshi Polisi mkoani Kilimanjaro linastahili pongezi na siyo lawama, waendelee hivyo hivyo na hakuna msalie mtume katika masuala ya uhalifu na uvunjaji wa amani, tumejipanga vyema kukabiliana na majambazi,” alisema.

Haki za binadhamu, zitekelezwe sawa sawa kwa wote, wabaya na wazuri. Vinginevyo, hazina maana.  Tusipongeze Jeshi la Polisi kama hawana uwezo wa kuchunguza jinai, kukamata wahusika na kupeleka kesi zao mahakamani.