“Utawala bora unalipa.” Haya ndiyo maneno ya Bw. Bertie Ahern, Waziri Mkuu wa Ireland, kwenye hotuba yake kwa wananchi wa Ireland ambao wanaishi hapa Tanzania. Soma hotuba nzima kwa kubonyeza hapa.

Pia, kwenye hotuba hiyo aliwasimulia wageni kuhusu mkutano wake na Rais Kikwete.

I commended the President for the very strong statements he has made on the need to tackle corruption. He acted decisively, openly and publicly following the recent independent international audit on the Bank of Tanzania.

His message to the people of Tanzania, to fellow African countries and to the wider international community is clear: Corruption has no place in a democratic society.

Lakini Bw. Bertie alisahau kuwaambia kuwa wapinzani pale Ireland wamedai kuwa yeye hastahili kuwa Waziri Mkuu kwa sababu chombo kimoja cha dola kinamchunguza kwa kutolipa kodi ya mapato wakati alipokuwa Waziri wa…………. Fedha.

Chanzo cha uchunguzi huo ni uchunguzi mwingine unaohusu mipango ya ardhi. Uchunguzi, unaojulikana kama Mahon Tribunal, umegundua kuwa Bw. Bertie alipokea malipo ya thamani ya zaidi ya Euro60,000 kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali kati ya mwaka 1993-94. Bertie ameshindwa kueleza kwanini walimpa pesa kiasi hicho wakati alikuwa Waziri wa Fedha.  Sasa mamlaka ya kodi ya Ireland wanamchunguza pia kujua kwanini hakulipa kodi ya mapato kwenye malipo hayo. Maelezo zaidi yanapatikana hapa.

Zaidi ya hapo, Bw. Bertie alifagilia umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari alipozungumza na wahariri wa magazeti mbalimbali ya Tanzania. Lakini nilishangaa Bw. Bertie alikataa kujibu swali lolote kuhusu madai ya wapinzani wake wakati wa ziara yake.

Mbona wafadhili wanatufundisha mambo ya utawala bora wakati wao wenyewe wanachunguzwa?